Ijumaa , 24th Jan , 2020

Mrembo Gigy Money amefunguka na kusema, katika maisha yake yeye ndiyo aliutaka umaarufu tangu zamani, pia umaarufu ulimfuata wenyewe baada ya kuwa kwenye mtandao wa Instagram.

Picha ya msanii Gigy Money

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Gigy Money amesema baada ya kuingia kwenye mtandao wa Instagram na kupiga picha za nusu utupu, ndiyo umaarufu wake ukakua zaidi.

"Mimi niliutaka umaarufu, huwezi kusema jambo limekutaka mwenyewe  kwani  halijanifuata nyumbani, umaarufu ulinifuata baada ya kuwa instagram nikajulikana baada ya kupiga picha za nusu ya mwili ukiwa wazi, lakini baada ya kuwa maarufu nikabadilisha brand yangu" amesema Gigy Money.

"Kama una nyota ya kujulikana na kuwa staa utajulikana tu, huwezi kuzuiliwa kwa chochote, sababu ya kuwa staa nayo ni kazi sio kila mtu ambaye anaweza, kuwa nacho hiko ni kapaji, ndiyo maana kuna wengine wanaenda kwenye mashindano yakutaka wawe maarufu" ameongeza.