"Kuna watu walijua sisi ni viziwi kweli"-Carpoza

Ijumaa , 10th Jan , 2020

Wachekeshaji wanaofanya vizuri kwa sasa hapa nchini Oka Martin na Official Carpoza, wamesema kuna watu walidhani kama wao ni viziwi kweli, kutokana na vichekesho vyao wanavyovifanya kuonesha kuwa ni viziwi.

Oka Martin upande wa kushoto, kulia ni Official Carpoza

Wakipiga stori na EATV & EA Radio Digital, wamesema mawazo ya kuchekesha kama viziwi yalikuja wakati wanapiga stori na mmoja wao akaja na kauli ya 'Unasemaaa' ndipo hapohapo wakaanza kurekodi video na kufanya kama wana matatizo ya kusikia.

"Tulikuwa katika mihangaiko yetu ya stori ikaja ile kauli 'unasemaaa' ndipo ilipozalishwa pale, tukafanya hivyo na bahati nzuri mtaani ikapokelewa vyema, kuna watu wengi waliamini kama sisi ni viziwi, walihisi ni kweli hatusikii vizuri" wamesema Oka Martin na Carpoza.

Wawili hao wameongeza kuwa "Kwa wageni wengi walidhania hivyo ila kwa watu wanaotufahamu tangia mwanzo ilikuwa sio rahisi kujua kama sisi ni viziwi kweli, ukiangalia vichekesho unaweza ukaamini, lakini ukija kwenye ukweli wetu unaona vitu vingine tofauti na utabaki kusema kumbe tunaigiza tu" ameongeza Oka Martin.

Pia wamesema muunganiko wao wa kufanya vichekesho hivyo, ulianzia studio walipokutana kwa sababu kabla ya kuingia kwenye vichekesho walikuwa wanafanya muziki wa HipHop.