Jumapili , 16th Dec , 2018

Msanii wa kike katika kiwanda cha Bongo Fleva, Mwasiti amesema kuwa kwa sasa hawezi tena kudanganya katika 'interview' kuwa yuko single kama zamani kwasbabu ya umri wake.

Mwasiti na Roma

Akizungumza kwenye Friday Night Live (FNL) ya EATV, Mwasiti amesema kuwa wanamuziki wengi wa kike hasa miaka ya nyuma walikuwa wanaogopa kusema ukweli kuwa wana mahusiano kwa kuhofia kuwa wataonekana tofauti na wengine wakihofia kutopata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wanaume, lakini kwa sasa ni tofauti na sio jambo la ajabu kwa mwanamuziki wa kike kumtaja mpenzi wake.

"Niko kwenye mahusiano, niko kwenye mahusiano mazuri tu na nina furaha, kwa umri niliofikia kila siku kwenda kwenye 'Interview' na kusema niko single ni uongo, ina maana hata hufuatwi na wanaume?," amesema Mwasiti.

Pia amezungumzia kazi yake mpya aliyomshirikisha Roma inayojulikana kama 'Fall in love' kuwa imekwenda vizuri kutokana na Roma kutaka uhalisia zaidi katika video, ndiyo maana katika 'scene' nyingi wameonekana kama ni wapenzi.

"Sehemu nyingi mnazoziona sio kama tulikuwa tunaigiza, tukicheka tunacheka kweli, ilikuwa nzuri kwasababu Roma alikuwa anataka uhalisia kwenye video. Alikuwa anataka watu waache zile kwamba wewe mume wa mtu unafanya Bongo Fleva basi huwezi kufanya kazi na mwanamuziki wa kike na mkafanya vitu ambavyo wanafanya wapenzi," ameongeza.