Jumanne , 26th Mei , 2020

Hakuna wimbo mbaya kama wa mwizi hasa akiimbiwa kutoka kwa raia ambao wamemzunguka katika mazingira aliyopo, na hujawahi kumuacha mwizi yeyote salama zikishapigwa hizo kelele.

Msanii wa Mduara AT

Sasa msanii na mkali wa muziki wa mduara AT amesema, kule kwao Zanzibar mwizi hapigwi bali watu wakisikia kelele za mwizi hutoka kumuangalia huyo mwizi yupoje au ana miguu mingapi.

"Ilinichukua miaka miwili kuzoea maisha ya huku bara, maana nilingia Dar es Salaam mwaka 2007, nilikuwa nahofia sana kuhusu wizi na ilinipa sana hiyo changamoto, kule kwetu Zanzibar mwizi hapigwi ila ukiita mwizi watu wanaenda kumuangalia huyo mwizi ndiyo nani na yupoje, na inaweza kupita hata miaka 15 usisikie kelele za mwizi" amesema AT