Lulu Diva aweka wazi msimamo wake akipokea uteuzi

Jumamosi , 21st Mar , 2020

Msanii wa Bongofleva Lulu Diva amesema yeye binafsi hana mpango wa kwenda kugombea ubunge nyumbani kwao Muheza Tanga, lakini yupo tayari kuwa mbunge endapo akiteuliwa na Rais.

Msanii Luludiva

Akiongea kwenye Friday Night Live, Lulu Diva amekiri kuwa hajawahi kufikiria kuingia kwenye siasa wala kugombea lakini akipata uteuzi anakweda bila kusitia.

'Mimi mambo ya siasa yamekaa kando lakini Mh Rais akiniona akasema Lulu diva una vigezo vyote akaniteua nikasimamie Muheza, mimi ni nani nikatae?', amesema Lulu diva.

Lulu kwa sasa ameachia EP yake yenye ngoma nne na ameiita jina 4some.

Tazama Video hapa