Lwaga amchumbia mpenzi wake "Wajumbe wawe wapole"

Jumatatu , 27th Jul , 2020

Muimbaji wa Injili aliyetamba na wimbo wake wa sitabaki nilivyo Joel Lwaga amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Muimbaji wa Injili Joel Lwaga na mpenzi wake

Tukio hilo limefanyika Julai 26,  limehudhuriwa na watu maarufu kama MC Pilipili ambaye alipost picha na video ya tukio hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram pamoja na MC Luvanda.

Akizungumza na EATV & EA Radio mara baada ya kumchumbia mpenzi wake huyo Joel Lwaga amesema kuwa "Kuhusu ndoa watu wasubiri tamko langu, hayo ni mambo binafsi na nyeti kwa sababu yanahusiana na familia, kwa misingi  yetu ya imani kuvisha pete ni hatua ya mapema ambayo haihitaji presha wajumbe watulie kidogo"

Zaidi tazama tukio lenyewe hapa chini.