Jumamosi , 28th Mar , 2020

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Mwasiti amesema ngoma yake na Chid Benz 'Hao' ndiyo ngoma ambayo ilimpa mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake ya muziki ambapo kupitia wimbo huo ilimuwezesha kufanya tamasha kubwa Afrika mbele ya Marais wengi barani Afrika.

Mwasiti amezungumza hayo kwenye kipindi cha Dadaz cha EATV ambapo amesema wakati akifikiria kutoa ngoma hiyo na Chid Benzi uongozi wake wa kipindi hicho haukuwa tayari.

"Nakumbuka wakati naupeleka wimbo wangu na Chid Benzi kwa Bosi wangu, aliniambia ule wimbo haukua level yangu, ila alipo ruhusu upigwe, ndani ya wiki moja tu ikanifanya kuwa Msanii mkubwa Afrika kwa sababu nilipata nafasi ya kwenda kufanya Tamasha kubwa Ethiopia mbeleya Marais wote Afrika" amesema Mwasiti

'Baada ya hayo mafanikio nikaamua kuwa Mwasiti wa sasa japo kuna wasanii wananiona mimi mshamba.' ameongeza Mwasiti

Tazama hapo chini