Jumatatu , 16th Jul , 2018

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu hadi Julai 20, 2018 siku ya Ijumaa kwa ajili ya kutoa uamuzi juu ya kesi hiyo.

muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu

Hayo yameelezwa mbele ya Mahakama hiyo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kusema sababu kubwa ya kesi hiyo kuhairishwa ni kutaka kupata muda wa kupitia baadhi ya vitu vinavyohusiana na kesi ya msanii huyo.

Baada ya maamuzi hayo kutolewa Mahakamani leo Julai 16, 2018 www.eatv.tv ilifanya jitihada za kumtafuta Wakili wa Wema Sepetu, Alberto Msando na kusema kwamba kwa sasa hawezi kuzungumza jambo lolote dhidi ya kesi hiyo.

Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bhangi, na kesi hiyo imehairishwa Julai 20, 2018.