Jumatano , 13th Nov , 2019

Msanii wa filamu na muziki Bongo Hemedy PHD,  ameiambia EATV & EA Radio Digital kuwa sababu ya kuzaliwa mzuri 'Handsome Boy' ni kutokana na mama yake kujifungua huku akiwa anakunywa kinywaji.

Hemedy PHD

Hemedy PHD amejibu suala hilo kutokana na watu kumchukulia kama mtu anayependa sana wanawake yaani 'Play boy'.

"Hapana sipendi wanawake, najipenda mimi mwenyewe tena najipenda sana kuliko kitu chochote na upendo unaanza na mimi kwanza. Watu wanaongea sana na kila mtu anaongea lake si unajua tena ukizaliwa 'handsome boy', mimi Mama yangu amenizaa anakunywa kinywaji kwa hiyo ndiyo maana nimetokea hivi mauzo mengi.", amesema Hemedy PHD.

"Kwa hiyo watu hawapendi kila mtu ataongea lake ila mwisho wa siku watu ambao nipo nao na naishi nao, wanaofuatilia maisha yangu na kuijua thamani yangu wanajua mimi ni nani kwao na namaanisha nini, sijali nani atawaza nini au Hemedy ni nani na anafanya nini.", ameongeza.

Pia Hemedy ameendelea kusema anachojua yeye kwenye maisha yake ni kula, kuvaa, kuhakikisha watoto wake wanapendeza na mama yake ana furaha kwani hiyo ndiyo baraka kwake.