Jumatatu , 28th Sep , 2020

Msanii wa BongoFleva Marioo amenyoosha maelezo kuhusu kutaka kujinyonga kisa kutendwa kwenye suala zima la mapenzi kama ambavyo alivyoashiria kwenye picha alizopost kwenye mtandao wa Instagram.

Msanii Marioo upande wa kulia, kushoto ni picha ya kitanzi ambayo aliipost kwenye mtandao wa Instagram

Marioo amejibu hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya siku ya jana kupost picha mbili ikionyesha vitanzi vya kujinyonga huku akiyalaumu mapenzi kwenye maneno ambayo ameyaandika. 

"Post zangu mbili tatu ndiyo zimeleta utata kidogo hadi watu kuanza kujiuliza, siku ya kwanza nilipost kitu nikiuliza hivi mapenzi ni kitu gani halafu baadaye nikapost vitanzi ambapo ikaleta utata mkubwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwamba Marioo anataka kujinyonga lakini sio kweli ile ni picha tu niliyotumia kwenye cover ya wimbo wangu

Aidha Marioo ameongeza kusema "Picha ile ilimaanisha kuwa namuongelea mtu ambaye amekata tamaa ya mahusiano hadi kufikiria kujinyonga kwa hiyo nikaamua kuweka kitanzi"