Martin Kadinda azungumzia uhusiano wake na Wema

Alhamisi , 4th Apr , 2019

Aliyekuwa meneja wa mwanadada Wema Sepetu, Martin Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi nchini amesema kuwa kutoonekana muda mwingi na Wema haimaanisha hawana mahusiano mazuri.

Martin Kadinda akiwa na Wema.

Martin amesema kuwa Wema amekuwa sasa hivi anatakiwa ajiongoze mwenyewe kwa kutumia elimu yake aliyonayo kuendesha biashara yake.

"Unapokuwa na elimu naamini ni rahisi kufanikiwa kwenye vitu unavyofanya kwakuwa changamoto utazichukulia katika hali chanya, hutokuwa mwepesi wa kukata tamaa, hivyo basi Wema ni mwanadada msomi na anaweza fanya hivyo kwani amekuwa sasa anatakiwa kujiongeza", amesema Kadinda.

Akizungumzia mwenendo wa Wema amesema kuwa sasa hivi mwanadada huyo anamuona katulia tofauti na awali ambapo alikuwa hakaukiwi matukio.