"Maziwa yanafanya nisiachane na Mke wangu"-Zumo

Ijumaa , 14th Feb , 2020

Kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 7:00 mchana -10:00 jioni, kimepiga stori na mchekeshaji Anko Zumo ambaye amesema mapenzi yake yamedumu kwa kunogeshwa na maziwa ya mkewe Habiba Zumo.

Picha ya Anko Zumo na mke wake Habiba Zumo

Anko Zumo amefunguka hilo kupitia  msimu huu wa wapenda nao na Nogesha Mahaba, ambapo amesema sababu ya kukaa kwa muda mrefu na mkewe ni kunyeshwa maziwa ambayo mpaka leo yamefanya wamefikisha miaka 8.

"Mwanzoni mimi na yeye tulikuwa hatuonekani pamoja japo mapenzi yalikuwepo, huyu ni mke wangu wa tatu, wa kwanza tulikaa miaka mitano wa pili tulikaa mwaka mmoja tukaachana, ila naona huyu ameniweza maana hata akinikera hatuachani, nafikiri ni yale maziwa ambayo yamenogesha kwa sababu tumekaa muda mrefu kwa miaka 8" ameeleza.

Aidha akizungumzia kuhusu utofauti aliouna kwa mke wake huyu wa sasa na hao ambao waliopita Anko Zumo ameongeza kusema.

"Utofauti niliouona kwanza kabisa huyu ni mvumilivu, cha pili ni kitendo cha kulea watoto wangu wote wawili vizuri japokuwa sio wa kwake, tatu haendekezi sana mahaba".