Meek Mill alivyougua ugonjwa uliofanana na Corona

Jumatano , 25th Mar , 2020

Rapa Meek Mill ameeleza kuwa aliumwa ugonjwa kama huu wa Corona mwishoni mwa mwaka jana, Disemba karibia na sikukuu ya Christmas ambapo alipoteza kilo 15.

MwanaHipHop Meek Mill

Akitumia mtandao wa Twitter kutoa taarifa hiyo Meek Mill amesema, hakuwahi kuumwa kama vile, pia hata madaktari walishindwa kuutambua ni ugonjwa gani unaomsumbua na kwa wazee ni hatari zaidi hawawezi kukabiliana nao.

"Niliumwa kama hivi mwezi Disemba karibia na sikukuu ya Christmas, nilikuwa na mafua yenye dalili za ugonjwa kama huu ambapo nilipoteza kilo 15, sikuwahi kuumwa kama vile na  sikuweza kufanya chochote, madaktari walishindwa kujua nini tatizo na kila siku nasema mtu mzee hataweza kukabiliana na ugonjwa huu"  ameandika Meek Mill.

Hapa Tanzania ni msanii mmoja tu wa HipHop ambaye ni Mwana Fa amejitokeza kusema amepata ugonjwa huo wa Corona ila sasa hivi yupo karantini na anaendelea vizuri.