Msanii Alikiba upande wa kushoto, kulia ni Meneja wa wasanii Max Rioba
Akipiga stori na eNewz ya East Africa TV, Max Rioba ameeleza kuwa sababu za kutamani kufanya kazi na Alikiba ni aina ya uimbaji wake ambapo anaamini itakuwa nzuri kibiashara kwa upande wao.
"Sasa hivi ukiniambia niwe meneja wa Alikiba nitafurahi sana kwa sababu najua yupo sehemu ambayo tutatengeneza mawazo ambayo yatajenga, kuleta pesa na kuuboresha huu muziki, natamani sana kufanya naye kazi kwa sababu jamaa ni muimbaji sana na anaweza, njia zake anazoenda yeye anaona kama zinafaa lakini naamini kuna haja ya ladha fulani hivi ambapo kwake hakipo" - amesema Max Rioba
Aidha Max Rioba amesema muziki wa sasa unaboa kwani wote wanaimba style moja ndiyo maana haudumu, pia meneja huyo liwahi kufanya kazi na msanii Young Dee miaka ya nyuma.
Zaidi mtazame hapo chini akijimwambafai.