Mfahamu Mtanzania aliyeigiza kwenye Game of Throne

Jumanne , 19th Feb , 2019

Imezoeleka kuona watu wa kutoka mataifa mengine wakifanya vizuri kwenye tasnia ya filamu duniani kupitia kiwanda cha filamu nchini Marekani Hollywood, lakini ni mara chache sana kuona watu kutoka Afrika wakifanya vizuri.

Hii imekuwa tofauti sasa, kwani hata Tanzania ambayo imezoelekea kukaa nyuma kwenye tasnia ya burudani dunaini, imefanikiwa kupenyeza mtu na kuipeperusha vyema bendera ya nchi, japokuwa sio moja kwa moja.

Anaitwa Lucian Gabriel Wiina Msamati, aliyezaliwa Machi 5 1976 huko Uingereza, ambaye wazazi wake ni Watanzania kabisa wakifanya kazi katika kada ya afya, huku akiwa mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne.  

Elimu yake ya msingi aliipata hapo Olympio jijini Dar es salaam, na kisha wakahamia Harare Zimbabwe, na kusoma katika shule ya Avondale, kisha kuendelea na elimu yake ya juu huko huko Zimbabwe.

Baada ya hapo Msamati alianza kazi kwenye 'media' kama mwandishi wa habari wa kujitegemea na kwenye kampuni mbali mbali za matangazo, huku akijihusisha na sanaa za majukwaani (theatrical).

Alipoanza kupata mafanikio kwenye sanaa ya filamu, Msamati alipata deals mbali mbali za kuigiza kwenye filamu kubwa kama Doctor Who, Luther, na Game of Throne ambayo bado inaendelea kutengenezwa muendelezo wake.

Kwa sasa Msamati amehamia nchini Uingereza na anaishi huko, tangu alipofanya uamuzi huo mwaka 2003, na kufanya kuwa mmoja wa waigizaji wakubwa wenye asili ya Tanzania, ambao nchi inapaswa kujivunia.