"Mimi ni nusu Mwanaume" - Gigy Money

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Staa wa Muziki nchini Gigy Money, ameitaja sababu iliyopelekea kujiita jina la  'King Gigy', ambalo aliwahi kulitumia katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram,kabla ya kulitoa siku za hivi karibuni.

Gigy Money

Akifunguka sababu hizo kupitia EATV & EA Radio Digital, Gigy Money amesema kujiita jina hilo ni maamuzi yake na maisha yake anayaendeesha mwenyewe bila kutegema danga au mtu mwingine yeyote.

"Yaani hata leo ingekuwa siku ya kina baba duniani ningeji-post mwenyewe, mimi ni nusu mwanamke na nusu mwanaume, kwa hiyo mimi ni Mfalme ni maamuzi ya kujiita jina hilo pia ni mwanamke ambaye najimiliki mwenyewe, sihudumiwi, sina danga wala sijawahi kudanga na haitakuja kutokea" amesema Gigy Money.

Pia amezungumzia kuhusu utaratibu wa watu wengi na baadhi ya mastaa kufanya "Birthday Party", ambapo kwa upande wake amesema.

"Sijawahi kufanya Birthday na sitofanya kwasababu sina pesa hizo, labda itokee kwenye siku hiyo watu walipe pesa waje kuniona, ila kwangu mimi kila siku nazaliwa na nilichaachaga kuwepo duniani naishi tu", amesema Gigy Money.