Jumamosi , 4th Jul , 2020

Captain wa BongoFleva Tunda Man amenyoosha maelezo kuhusu mke wake kupokonywa gari na Chief Kiumbe, gari ambalo alimzawadia kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkewe huyo mwaka jana 2019.

Msanii wa BongoFleva Tunda Man akiwa na mkewe Sabra

Akizungumzia hilo Tunda Man ameeleza kuwa mkewe hajapokonywa gari ila kilichotokea ni kumuuzia gari Chief Kiumbe baada ya mke wake kudai gari hilo linamzidi kimo na linampa shida.

"Gari nilimuuzia Chief ninao hadi mkataba wa kumuuzia hadi pesa sijamaliziwa kama milioni 7 au 8 hivi, gari alitembea nalo mke wangu ila aliligonga na lilimzidi kimo tukalipeleka kwa fundi kisha Chief akalipia kulinunua,sasa hivi nimemnunulia gari nyingine yenye thamani ya Milioni 22, kwa sasa hivi Chief amekwama Afrika Kusini kwa sababu ya Corona ila alipanga akirudi aje kunimalizia" ameeleza Tunda Man