Jumamosi , 16th Feb , 2019

Msanii Chidi Benz amesema kwamba kitendo cha watu kuwapaisha wasanii wasio na uwezo mkubwa na kuwaacha wale wenye vipaji vikubwa ni kibaya, kwani ni sawa na kumuua mtu.

Akitolea mfano kati ya wasanii wawili wa Bongofleva Alikiba na Jux, Chidi Benz amesema kwamba iwapo utampaisha Jux zaidi na kumuacha Alikiba, ni sawa na kumuua Alikiba kiakili, kwani wawili hao hawawezi kulinganishwa kulingana nauwezo mkubwa laionao Alikiba.

“Jux sio msanii mkali, wanachomfanyia hawamfanyii hata Alikiba, mnamuua Alikiba kwa mawazo, mnachamnganya Alikiba kiakili, mnamtengua Alikiba kikazi, anakuwa anamuwaza waza Jux, watu wanamuangalia Jux, mnawaua waimbaji”, amesema Chidi Benz.

Kutokana na hilo Chid Benz amewataka kusapoti kazi za watu wenye vipaji kweli na kuacha kubagua kwa sababu yoyote ile, ili game iweze kukua zaidi na kuokoa wasanii wenye uwezo kutoanguka.