Jumatatu , 28th Oct , 2019

Mrembo na Mama wa watoto wawili, Hamisa Mobetto,amesema kuwa kwa sasa yupo 'single' na hana muda wa kumpa binadamu mwingine, pamoja na kutolea ufafanuzi juu ya video yake iliyosambaa mitandaoni, ikionesha anamkatikia viuno mwanaume mmoja ambaye hajajulikana kwa jina wala sura.

Kupitia  EATV & EA Radio Digital, Hamisa Mobetto, amesema ameamua kuwa single kwa sababu ana mambo mengi ya kufanya na anaona muda hautoshi wa kumpa binadamu mwingine.

 "Mimi nipo single, sina mpenzi na sipo tayari kuingia kwenye mahusiano na sio kama sitongozwi au sina watu ambao wanataka kuwa na mimi ila kwa sasa nipo bize sana na mambo yangu, nafanya kazi nyingi sana naona muda kama hautoshi na siwezi kuwa na muda mwingine wa kumpa binadamu zaidi ya watoto wangu na familia yangu" amesema Mobetto.

Aidha akizungumzia video iliyosambaa mitandaoni, ikimuonesha akimkatikia mwanaume amesema.

"Tulikuwa club na yule ni rafiki yangu kwahiyo ni mambo ya kawaida tu sijui kwanini ilikuwa ni jambo kubwa kwa sababu naamini kila mtu anacheza na sikutegemea kama itatrend ila ni kawaida, nilikuwa nacheza nyimbo tu hakuna cha mpenzi wala kitu kingine" ameeleza Hamisa Mobetto.