Mpenzi mpya wa Dogo Janja apewa kisomo

Jumanne , 11th Feb , 2020

Rais wa Manzese Madee Seneda, amemshauri mpenzi mpya wa Dogo Janja "Quenlinnah" kwa kumwambia ategemee mengi kwa sababu yupo kwenye mahusiano na mtu maarufu.

Picha ya Dogo Janja akiwa na mpenzi wake Quenlinna Toto

Madee amesema hayo baada ya Dogo Janja kumvalisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo siku ya jana Februari 10, 2020, kwenye boti wakati wanarudi Dar es Salaam wakitokea visiwani Zanzibar.

"Mpenzi wa Dogo Janja ajue kabisa yupo kwenye mahusiano na mtu maarufu na yeye anaelekea kuwa maarufu muda sio mrefu, kwahiyo asisikilize maneno ya watu na ategemee mengi ambayo yatatikisa mahusiano yao ambayo ni mapya" amesema Madee.

Aidha katika msimu huu wa wapendanao Dogo Janja mwenyewe amesema "Msimu wa mapenzi umekuwa mzuri kwetu kwani nimeufurahia sana mimi na mpenzi wangu kule visiwani Zanzibar, nikiwa na familia yangu kama Linah, Recho na Madee".