Ijumaa , 18th Oct , 2019

Mwanamuziki wa Injili Joel Lwaga, amefunguka na kusema yeye ana uwezo wa kwenda kwenye Kanisa la Mlima wa Moto kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji na maombi, lakini si kwa kupelekwa na upepo wa Kisulisu

Joel Lwaga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni, kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na Youtube ya East Africa TV, kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana.

"Kwa Mama Rwakatare pale Mlima wa Moto nitaenda kuhudumu lakini sio kupitiwa na upepo wa Kisulisuli"amesema Lwaga.

Aidha kwa upande wake, Mchungaji wa Mlima wa Moto Getrude Rwakatare, amesema lengo la ujumbe huo ilikuwa ni kuwaombea wanaume huko walipo wakutwe na nguvu ya ajabu ya kiroho, ili waweze kufika kanisani kwake na kuwaoa wanawake ambao hawana waume.