Jumatatu , 11th Nov , 2019

Msanii wa kike wa muziki wa BongoFleva Wini Tz, amesema kuwa mara nyingi nguo zake anazovaa, hutumia zaidi ya shilingi milioni 1 hii inatokana na yeye kupenda kuvaa vitu vizuri zaidi.

Msanii wa kike wa muziki wa BongoFleva Wini.

Wini Tz amelazimika kutaja gharama hizo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuwa anatumia shilingi ngapi hadi kutengeneza muonekano mzuri kupitria mavazi yake.

"Gharama ni nyingi sana tukianza kuhesabu itakuwa sio poa, kila kitu kipo katika viwango, jumla ni zaidi ya milioni moja, napenda kuvaa napenda kupendeza kuonekana vizuri ni kitu kilichopo ndani yangu kama ilivyo muziki, hata kama utanikuta nyumbani nipo vizuri" amesema Wini Tz.

Aidha Wini Tz ameongeza kuwa mara nyingi anunuapo vitu vyake, hutoa hela yake mwenyewe na si kumtegemea mwanaume, "Itategemea na sehemu ninayokwenda inaweza ikawa zaidi ya milioni au pungufu ya hapo, ila kwa mavazi ya beach siwezi kutumia pesa nyingi".