Ijumaa , 21st Feb , 2020

Staa wa muziki hapa nchini Alikiba ameonekana  akiwa pamoja na familia yake ambao ni mke wake Aileenalora na mtoto Keyaan Alikiba,  baada ya taarifa zilizoripotiwa mwishoni mwa mwaka jana kwamba ametangana na mke wake huyo.

Picha ya Alikiba akiwa na mkewe pamoja na mtoto wao Keyaan

Kupitia mtandao wa Snapchat Alikiba alirekodi video fupi ikimuonyesha  mkewe huyo pamoja na mtoto wao ambao wameonekana wakiwa na furaha.

Aidha siku mbili zilizopita mtoto wao huyo alikuwa anasheherekea kumbulumbu ya kutimiza umri wa miaka miwili ambapo taarifa zinasema hiyo ndiyo sababu ya wazazi wake kuonekana tena wakiwa pamoja.

Pia kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Alikiba amem-follow mtu mmoja tu ambaye ni mwanaye Keyaan Alikiba, msanii huyo huwa hanaga utaratibu wa kumfollow mtu yeyeote kupitia mtandao huo.