Muziki una masharti yake - Rama Dee

Jumatano , 26th Jul , 2017

Mkali wa R&B Rama Dee amefunguka kwa kudai sababu kubwa inayopelekea muziki anaoufanya yeye kukosa waimbaji wengi kama ilivyokuwa sehemu nyingine ni kutokana na muziki huo kuwa na mahesabu mengi jambo ambalo pengine linawafanya washindwe kuingia.

Mkali wa R&B Rama Dee.

Rama D amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV baada ya kuonekana na pengo kubwa katika muziki wa aina hiyo kutofanywa vizuri nchini Tanzania ukilinganisha na nyimbo nyingine zinazotolewa kila siku.

"Kila muziki una masharti yake hata singeli una masharti vile vile kwa hiyo inawezekana labda 'arts' wengine hawajapendezwa na muziki wa R&B ndiyo maana wanashindwa kuingia. Kwa sababu R&B lazima ufanye mahesabu kidogo, uzingatie misingi kwa sababu sijawahi kumuona mtu akiimba kitu ambacho haki 'make sense' katika jamii kwa ujumla. R&B inaendana sana na 'Hip hop' ni muziki ambao upo 'positive' zaidi katika kuelimisha jamii kwa ujumla", amesema Rama Dee.

Kwa upande mwingine, Ram Dee amesema amekuwa hafanyi 'show' bongo kwa kuwa anatafuta watu wa kumsaidia kutengeneza show nzuri na siyo bora show ili kusudi shabiki zake waweze kubakia na historia.

Mtazame hapa anavyofunguka zaidi.