Mwana FA asema Yanga ndiyo timu pekee duniani

Jumapili , 28th Apr , 2019

Rapa anayefanya vizuri kwa muda wote, Binamu 'Mwana FA' na Shabiki wa Simba, ameshangazwa na watani zake Yanga kwa kauli zao za kinyonge huku wakiwa ndiyo vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mwana FA

Mwana FA amelazimika kuyasema hayo kutokana na mwendelezo wa kauli kutoka kwa watani zao wakilalamikia Simba kubebwa katika michezo ya Ligi Kuu inayoendelea.

"Ndala (Yanga)  ndio timu pekee duniani wanaoongoza ligi lakini wanatoa kauli za kinyonge kama ‘tujipange kwa mwakani tu wazee", ameandika FA.

Yanga kwa sasa tayari wamekwisha cheza mechi 32 wakiwa kileleni kwa pointi 74, Simba ikishika nafasi ya pili ikiwa imecheza michezo 27 na pointi 69 huku Azam ikishika nafasi ya tatu na pointi 66.