Mwanasheria azungumzia kosa la Dudu Baya

Ijumaa , 1st Mar , 2019

Mwanasheia Jebra Kambole amesema kwamba kitendo alichokifanya Dudu Baya ni kosa kisheria, na amevunja kifungu cha 35 cha Sheria ya Huduma ya Habari ya Mwaka 2016, kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na www.eatv.tv, Jebra Kambole amesema kwamba kifungu hicho kinakataza kukashifu mtu hata kama ni marehemu, na iwapo mtu huyo atashtakiwa na mahakama kumkuta na hatia, basi anaweza akafungwa jela au akalipa faini.

Kwa mujibu wa sheria zetu sisi ni kosa la jinai lakini pia linaweza likawa kosa la madai, lakini kwa matusi ambayo yametolewa na mtu dhidi ya marehemu, sheria imeelekeza kwamba kama shtaka linafunguliwa mahakamani lazima kuwe kuna ridhaa ya DPP”, amesema Jebra Kabole.

Akiendelea kufafanua hilo Jebra Kambole amesema kwamba, “adhabu ya ukwiukwaji wa kifungu namba 35, na vifungu vyote vinavyohusiana na lugha ya kasha au ya matusi dhidi ya watu wengine au marehemu, inaeleza kwamba endapo mtu atapatikana ametenda kosa, anaweza akapewa adhabu ambayo haipungui milioni 5, au haizidi milioni 20, au anaweza akapewa kifungo kisichopungua miaka mitatu, au kisichozidi miaka mitano”.

Hivi karibuni msanii huyo mkongwe wa kizazi kipya alitakiwa kuchukuliwa hatua na jeshi la polisi ikiwa ni amri kutoka kwa waziri wa Habari, sanaa, utamaduni na Michezo, kwa kutoa lugha ya kejeli kwa mmoja wa waasisi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, ambaye amefariki Februari 26.

Msikilize hapa chini