Jumatatu , 30th Mar , 2020

Msanii wa kike anayefanya vizuri hapa nchini Tanzania Mwasiti, amesema kuwa mdhamini wa show yake ya kwanza kuifanya alikuwa ni mama yake mzazi, ambaye alimkopesha hela kwa maandishi na baadaye akata kurejeshewa.

Msanii wa kike Tanzania, Mwasiti.

Mwasiti ameyabainisha hayo kwenye kipindi cha DADAZ, kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa na kusema kuwa alipotaka kumrejeshea, mama yake aliikataa pesa hiyo.

"Kuna show nilipata lakini nilikuwa sina hata mia, ikabidi nimfate mama yangu nikamuomba anikopeshe, kwahiyo show yangu ya kwanza Sponsor alikuwa ni mama yangu, lakini alinidai hela yake baada ya kulipwa nikamrudishia lakini aliikataa kuipokea na kusema ameamua kunisaidia ili kutimiza ndoto yangu" amesema Mwasiti.

Aidha Mwasiti ameeleza faida ya msanii yeyote kuishi maisha yake, ambayo yatakuwa hayana utofauti na watu wengine wa kawaida, kwani hali hiyo yeye inamfanya kujichanganya kwenye makundi ya watu wote na kuwa huru zaidi.