Mzee afanyiwa tambiko baada ya kufumaniwa

Jumapili , 10th Mei , 2020

Mzee wa miaka 84 kutoka kaunti ya Bungoma nchini Kenya amelazimika kufanyiwa tambiko la kuchinjiwa kondoo baada ya kufumaniwa na mkwe wake wakifanya mapenzi.

Gari la polisi lililoenda kumuokoa baada ya tukio hilo

Mzee huyo ametambulika kwa jina la William Makhanu, amewashtua wanakijiji wa eneo lake baada ya kufanya tukio hilo na nia ya kufanyiwa tambiko kwa kabila lao la Bukusu ni kumtakasa na kuzuia laana kwenye familia.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wazee wa Bukusu Jared Barasa amesema "Kulingana na mila na desturi zetu ni makosa,  sisi kama wazee tutalazimika kumchinja kondoo kumtakasa pamoja na mkwe wake".

Aidha mmoja wa watoto wake aitwaye Wanjala amesema mzee wao aligoma kufungua mlango hadi walipolazimika kuuvunja akihofia adhabu ya kuchapwa viboko 20. 

"Tulimuamuru  aondoke chumbani ila alikataa  hadi tukalazimika kuuvunja mlango, kama wanawe tunahisi aibu kubwa kwa kuwa tuna wake na labda huenda amekuwa akiwatumia wote"

Chanzo Tuko News, Kenya