"Nahisi dalili za Corona" - Ebitoke

Jumatano , 25th Mar , 2020

Mchekeshaji Ebitoke ameeleza ana muda wa wiki 1 anajihisi mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Corona na anachotaka kufanya ni kuchukua hatua ya kwenda kupima ili kujua kama ana ugonjwa huo au hana.

Picha ya Mchekeshaji Ebitoke

 

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Ebitoke amesema tangu ugonjwa huo umeanza amechukua tahadhari za kupunguza misongamano na kushinda ndani, ila haelewi ugonjwa huo ameupatia wapi.

"Tahadhari za Corona ni kujikinga kwa kuvaa mask, kuepuka mikusanyiko ya watu na kushinda nyumbani, hapa nilipo nahisi nina dalili za Corona kwa asilimia maana nina shida mwilini, kwa kuwa nimeshakuwa na dalili hizi nitachukua hatua ya kupima ili nijue kama ninao au sina" ameeleza Ebitoke.

Pia ameendelea kusema "Imekaribia kama wiki hivi tangu kupata dalili hizi, japokuwa bado ninasikilizia ila nitakwenda hospitali ila tangu ugonjwa huu umeanza nimejikinga sana sijui hata umenipataje" ameongeza.