Jumanne , 19th Feb , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayejulikana kwa jina la Holy Star, amesema kwamba ana ndoto kubwa kwenye muziki wake, na sio kwa ajili ya watanzania tu, bali kwa dunia nzima na umuingizie pesa nyingi.

Akifunguka kuhusu hilo, Hollystar amesema kwamba anataka muziki wake ufike dunia nzima kiasi kwamba akisimama jukwaani dunia atambulike kama Holystar, na kuwa zaidi ya mfalme wa Pop duniani, Michael Jackson.

Malengo yangu ni kufika mbali, kupata pesa kupitia muziki, kuwa na maisha mazuri, nina mawazo makubwa, nahitaji kufika anga za kimataifa, sitaki kufanya muziki kwa ajili ya Dar es samaam au Watanzania, nataka kufanya muziki kwa ajili ya dunia nzima, nataka siku Holystar akisimama jukwaani awe more than Michael Jackson”, amesema Holystar.

Msanii huyo mpaka sasa ameachia kazi zake takriban tano, na amesema kwamba bado hajakata tamaa na muziki, kwania ana imani ipo siku atatoboa na kufika mbali zaidi.