Ijumaa , 21st Apr , 2017

Mwanamuziki anayesumbua kwa sasa na wimbo wa 'Wapo' Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego amejitetea kwenye eNewz ya EATV kuwa watu wasihusishe vitu anavyoweka kwenye mitandao ya kijamii na tukio la utekwaji wa msanii Roma Mkatoliki.

Nay amefunguka hayo baada ya kuulizwa kuhusu maneno aliyoyaweka kwenye mtandao wake wa Instagram siku moja baada ya kupatikana kwa msanii Roma pamoja na wenzake wanne ambao inasemekana walitekwa na watu wasiofahamika.

"Ni dhambi kubwa watu kuhusisha post zangu na tukio la Roma kwa sababu mimi sikumlenga mtu yeyote yule. watu wameamua kuunganisha tukio la Roma na post zangu kwa sababu ya mihemko waliyokuwa nayo. Mimi nina washkaji wachahe sana na Roma ni mshkaji wangu sana na ninaamini alipata matatizo kweli. Watanzania nao naomba wamuamini kwa kipindi hiki ambacho anauguza majeraha lakini pia wamsapoti tukianza ku-coment vitu vya tofauti tutaharibu hata carrier yake na yule ni msanii hii ndiyo ajira yake" - Alisema Nay wa Mitego.

Hii ndiyo post ya Nay iliyozua gumzo baada ya Roma kupatikana

Hata hivyo katika siku yake ya kwanza kuzungumza na wanahabari baada ya kupatikana, Roma pamoja na mambo mwengine aliwalalamikia baadhi ya wasanii ambao ni watu wake wa karibu kumzungumzia vibaya kuwa anatumika kisiasa na baadhi ya wanasiasa na hata tukio la kutekwa alilipwa dola 5000 kwa ajili ya kuwapumbaza wananchi.

Mtazame hapa Nay katika show ya eNewz