Nay wa Mitego aachana na Nini

Jumatano , 1st Mei , 2019

Msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego, ameweka wazi kuwa ameachana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye pia ni msanii wa Bongofleva Nini.

Wasanii Nini na Nay wa Mitego

Nay ameimbia eNews ya East Africa Television kuwa, kwasasa ametulia na mwanamke ambaye ni mtulivu na sio mtu wa mitandao wala vyombo vya habari hivyo ametulia na kuacha mambo mengi.

''Mimi na Nini tumeachana, sipo naye tena muda mrefu nina mahusiano yangu mengine na yana utulivu sana. Mimi huwa sijifichi ila kwasasa nimetulia na mwanamke kama wimbo wangu mpya unavyosema Nishaachaga'', amefunguka.

Nay ameongeza kuwa kwasasa anaangalia zaidi familia yake wakiwemo watoto wake kwani wameshakuwa wakubwa hivyo kuna baadhi ya mambo lazima aachane nayo.