Nay Wa Mitego amuomba Shamsa kurudi kwa mumewe

Jumanne , 31st Mar , 2020

Moja ya stori iliyotrend mitandaoni siku ya jana Machi 30, 2020 ni ya mfanyabiashara Chiddi Mapenzi, kumuandikia ujumbe wa kumkumbuka aliyekuwa mkewe Shamsa Ford na kujutia kumpoteza kwenye maisha yake.

Nay Wa Mitego na Shamsa Ford

Sasa wakati stori hiyo inaendelea kuzungumziwa, msanii wa HipHop Nay Wa Mitego, ametumia ukurasa wake wa Instagram na kumuomba Shamsa Ford, kumsamehe mumewe na kurudiana naye.

Kupitia post ambayo aliiweka na kuifuta Nay Wa Mitego ameandika kuwa,  "Cousin Shamsa Ford, wanasema samehe saba mara sabini, tafadhali msamehe mwenzio amekiri makosa, embu rudi kwa mumeo bana tafadhali, tafadhali rudi kwa mumeo"

Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma Nay Wa Mitego na Shamsa Ford, walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, kisha baadaye Shamsa Ford kufunga ndoa na Chiddi Mapenzi.