Nedy afunguka kumfulia nguo za ndani mpenzi wake

Jumanne , 24th Mar , 2020

Msanii Nedy Music ameeleza kuwa, huwa anamsadia mpenzi wake kupika, kuosha vyombo hata kumfulia nguo zake zote hata za ndani pia inawezekana.

Msanii Nedy Music

Nedy Music amesema, anafanya hivyo kutokana na thamani anayompa mwanamke wake kwa kuwa anamfanyia vitu vingi na yeye binafsi  hachagui kazi.

"Huwa nafanya vitu vingi kwa ajili yake, mimi ni mwanaume ambaye hata kwa mwanamke wangu naweza kumfulia nguo zake zozote ambazo yuko nazo bila kujali chochote, thamani yangu kwake ni kubwa kwahiyo hata nguo za ndani inawezekana kabisa kumfulia" amesema Nedy Music.

Aidha ameendelea kusema "Sidhani kama kumfulia mpenzi wako ni ishu kubwa, kama utaiangalia kiubinadamu na kiuwanaume" ameongeza.