Jumanne , 9th Oct , 2018

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume, amefunguka juu ya mapenzi yake juu ya msanii wa muziki wa bongo fleva, Nay wa Mitego.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Fatma Karume amesema anampenda sana Nay wa Mitego, kutokana na ubishiwake anaouonesha licha ya kukumbana na vikwazo vingi katika kazi yake.

“Kwenye Bongo Fleva nampenda sana Nay wa Mitego, I like that man(Ninamkubali sana), unajua binadamu ukisha kutandikwa, halafu ukasema to hell, ukarudi ukasema wapo, ni big respect (Heshima kubwa sana), kama unanisikiliza Nay, Ilove you”, amesema Fatma Karume

Fatma Karume ameendelea kwa kusema kwamba msanii huyo ameonesha ujasiri mkubwa kwa kuendelea kufanya muziki, licha ya kungiwa mara kadhaa, kitendo ambacho amekitaja kama uonevu.

Msanii huyo anatamba na wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la 'Alisema' ambao ameuachia wiki hii na kuzua mijadala kutokana na maneno aliyoyatumia.