"Nilijua tu singeli itakufa "- Msaga Sumu

Monday , 17th Jul , 2017

Msaga Sumu amefunguka na kusema alitambua mapema kwamba aina ya muziki wanaofanya utakufa mapema kwani wasanii wake hawana ushirikiano.

Akizungumza na Stori tatu ya Planet Bongo, Msaga Sumu amesema kwamba wasanii wachanga waliokuja kuibuka hivi karibuni ndio chanzo cha kupelekea singeli kupotea kwani walianza kutengeneza mabifu wao kwao badala ya kuboresha kazi.

"Nilijua muziki wa Singeli utakufa kwa sababu hatukuwa na ushirikiano, wenzetu wa bongo fleva wamefanikiwa sana mpaka wamejijengea majina makubwa ni kwa sababu wameweza kushikamana, Tatizo pia hawa watoto waliokuwa wametamba na nyimbo zao mbili mbili nao wakaanza kuwekeana mabifu na mwisho wa siku wamepotea wao walidhani wamemaliza", Msaga amesema.

Akizungumzia kwa upande wake kushindwa kuachia nyimbo mfululizo, Msaga Sumu amesema 

"Mimi niliacha kutoa nyimbo baada ya kuona tena kuna kuigana. Wasanii wanashindwa kuwa wabunifu kwa sababu na badala yake wote tukawa tunaonekana hatuna kitu chochote" aliongeza Msaga Sumu.

Msikilize hapa chini akifunguka zaidi.

Recent Posts