Alhamisi , 14th Feb , 2019

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Isabella ambaye leo amelazwa hospitali kutokana na msongo wa mawazo alioupata kutokana na kifo cha Godzilla, ameweka wazi kuwa kwenye mahusiano na Godzilla, amesema kwamba aliamua kuwa naye kwa sababu ya kulipiza kisasi baada ya kuachwa na mpenzi wake.

Akizungumzia hilo Bella amesema kwamba awali yeye alikuwa mchumba wa mtu na amezaa na huyo mwanaume, lakini  walipoachana akaamua kurudi kwa Godzilla, ili kulipiza maumivu ya kuachana na mzazi mzazi mwenzake.

Unajua mimi nilikuwa mchumba wa mtu, nikagombana na baba mtoto wangu, kwa hiyo na mimi revenge yangu nikarudisha mahusiano yangu na Zilla, ingawa tulikuwa wapenzi kabla tuliachana, baada ya kugombana na baba mtoto wangu nikaamua kurudiana naye na kwa vile tulikuwa tunaishi karibu huku Salasala. Jana nafsi yangu ikaona tu niseme ukweli, na sasa najisikia na amani”, amesema Isabella.

Kutokana na hilo Issabela amewataka watu wanaosema kuwa anatafuta kiki kuacha, kwani anachokiongea sio kiki bali ni ukweli ambao ameshindwa kuvumilia kuuficha, ingawa hawakuwa na plan zozote kwenye mahusiano hayo.