"Nondo amenichukiza, hatutaki virusi"-Baba Levo

Jumatatu , 6th Jul , 2020

Aliyekuwa Diwani wa Mwanga Kigoma Ujiji na msanii Baba Levo, amesema kuwa amechukizwa na kitendo cha Mwenyekiti wa ngome ya vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo, kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigoma mjini.

Msanii Baba Levo upande wa kushoto na Abdul Nondo upande wa kulia

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Baba Levo amesema hataki virusi katika jimbo lao na atapambana naye kuhakikisha analichukua jimbo hilo na ikishindikana bora aje alichukue mwenye jimbo lake  Zitto Kabwe.

"Nilisema kama Zitto Kabwe hatagombea mimi nitagombea, nitapambana na mtu yeyote atakayekuja Kigoma Mjini, lengo ni kuzuia virusi na watu ambao hawana sifa  za kuongoza, Abdul Nondo kutangaza nia ya kugombea ni Demokrasia lakini amenichukiza sana bora Zitto arudi kuchukua Jimbo lake wote tukose" amesema Baba Levo

Zaidi tazama kwenye Video hapa chini.