Ommy Dimpoz arejea hospitali Ujerumani

Jumapili , 28th Apr , 2019

Msanii wa Bongofleva Ommy Dimpoz, amethibitisha kurejea hospitalini huko Ujerumani kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Ommy Dimpoz akiwa hospitali.

Dimpoz amerudi Ujerumnai ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu afanyiwe upasuaji wa koo mwaka jana.

Hata hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ommy ameweka wazi kuwa uchunguzi huo umekwenda salama na amemshukuru Mungu kwa hilo. ''Alhamdulilaah Mungu Ni Mwema'' #CheckupsDone.

Ommy alikaa nje ya game kwa muda, kufuatia kusumbuliwa na tatizo la koo ambapo alianza kwa kupata matibabu nchini Kenya kisha Afrika Kusini na baadaye Ujerumani.

Licha ya kuendelea na muziki kwa kutoa ngoma tatu za ni Wewe, Your the best na Rock Star Ommy amekuwa akisisitiza kuwa hawezi kufanya show mpaka arudi kwa daktari apewe mwongozo. 

Hivyo baada ya uchunguzi huu tunaweza kumuona Dimpoz jukwaani.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Alhamdulilaah Mungu Ni Mwema #CheckupsDone

A post shared by Ommy Dimpoz (@ommydimpoz) on