Jumatano , 18th Mar , 2020

Moja kati ya stori ambayo inazungumziwa kwa sasa ni juu ya mahusiano kati ya msanii wa filamu Wastara Juma na Z Anto, ambapo watu wengi hawakutegemea kama wawili hao kama wangekuwa wapenzi.

Wastara Juma na Z Anto

 

Mahusiano yao yame-trend  zaidi  baada ya Wastara kumtishia kumchana viwembe mke wa zamani wa Z Anto, ambaye ni Binti Kiziwi kuwa aache kumtafuta mwanaume wake, hali iliyopelekea kuonekana wanamgombania mwanaume mmoja.

Kupitia EATV & EA Radio Digital, imempata Wastara Juma na amenyoosha maelezo kuhusu tukio zima la kumgombania Z Anto ambapo amesema.
 
"Nimetoa onyo mtu asimsogelee Z Anto kutoka sebuleni hadi chumbani, kwahiyo nimeweka kizuizi, nimemshambulia Binti Kiziwi kwa sababu ndiye aliyenifanya nimshambulie na wengine wajue kabisa wakija kumgusa wawe wamejipanga maana tutatoana macho"  amesema Wastara Juma.

Aidha ameongeza kusema  "Kumgombania ni suna kwa sababu nina wivu, ukiona mwanaume namgombania ujue ananiridhisha kwa kila kitu, mwanamke ambaye anaridhishwa na aliyepitia kwenye  mahusiano hawezi kukubali kumpoteza mtu wake".