Prezzo ashindwa kujizuia kwa Rais Magufuli

Jumanne , 8th Oct , 2019

Msanii wa Kenya na mfanyabiashara Prezzo, ameonekana kumsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na uongozi na utendaji wake wa kazi.

Msanii Prezzo na Rais Magufuli

Msanii huyo alipost video fupi katika mtandao wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha Rais Magufuli akimsaidia Mwanamke mmoja ambaye alishindwa kulipa pesa, ambazo alikuwa anadaiwa katika Hospital ya taifa ya Muhimbili.

"Hii ilini-touch, Africa tungekuwa na viongozi kumi kama Muheshimiwa Magufuli kwakweli tungekuwa mbali sana badala ya kupata taabu saaaana. Mwenyezi Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yako Your Excellency" aliandika.

Baada ya muda mfupi mashabiki walitoa maoni yao kuhusu video hiyo iliyopostiwa na Prezzo ambapo waliandika,

Eunice 8181 "Iliumiza wengi Sana, tuna Rais mwenye huruma Sana hasa kwa wanyonge".

John Maniha "Bonge la point bro. dingi huyu ni mashine na hana uoga kabisa, hata wazungu anawachana live bila kupepesa macho".

Asiimwe David "President magufuli mungu azidi kumlinda na pia akupe maisha mazuri more life mr president your humanity is a gift from God".

Ikumbukwe tu Prezzo ameingia rasmi kwenye siasa baada ya kutangazwa kugombea Ubunge katika kaunti ya Kibra iliyopo kusini mwa Jiji la Nairobi, msanii mwingine ambaye ameingia katika siasa ni Jose Chameleone kutoka nchini Uganda.

Kama watafanikiwa kushinda katika uchaguzi wao wataungana na wasanii ambao wapo kwenye uongozi wa siasa kama Prof. Jay , Joseph Mbilinyi "Mr II Sugu", na Jaguar kutoka Kenya.