Ijumaa , 22nd Jan , 2016

Mheshimiwa Joseph Haule, ambaye kwa upande wa sanaa anafahamika kama Proffesa Jay, akiwa sasa ni Mbunge anayeliwakilisha vizuri jimbo la Mikumi amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya bunge ya UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC).

Mhe. Joseph Haule

Katika ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ameweka taarifa hizo kuonesha furaha yake, akiongeza pia na ujumbe "Mdogo mdogo Tutafika!" kumaanisha kuwa safari yake bado inaendelea kufikia mafanikio zaidi na zaidi.

Msanii huyo atakuwa akifanya kazi na wabunge wenzake katika kamati hiyo akiwepo Mheshimiwa Ester Nicholas Matiko wa Tarime Mjini, Mheshimiwa Sabreena Hamza Sungura wa Viti Maalum, Mhe. George Kakunda wa Sikonge, Mhe. Sannda Mgante wa Kondoa Mjini na Mhe. Fatma Hassan Toufiq wa Viti Maalum.