Jumanne , 29th Sep , 2020

Msanii wa kundi la The Mafik Rhino King amesema anapenda kupaka rangi kucha zake kwa sababu ni mtindo wa pekee, na hataki watu wamuingilie kwenye maisha yake binafsi japo baadhi ya watu wamekuwa wakimshambulia kutokana na kitendo hicho.

Msanii wa BongoFleva Rhino King

Akifunguka kupitia eNewz ya East Africa TV Rhino King amesema “Kupaka rangi katika kucha zangu kwanza familia yangu hawajaliongelea hilo inakuwaje watanzania kuliongelea, nilianza kupaka rangi kabla sijakuwa mbele ya vyombo vya habari, sio kitu cha kuwapa watu attention, style ya kupaka rangi kucha kwangu ni ya kipekee"

Mtoto wakiume kupaka rangi kwenye kucha ni sawa tu na wa kike kupaka rangi watanzania wayaache tu maisha yangu mengine hata mwanzo nilikuwa na dread kichwa kizima sasahivi nina dread upande mmoja  maisha yanabadilika watu wajifunze kuwa kila mtu na maisha yake” ameongeza