Jumatatu , 27th Jan , 2020

Mtunzi wa mashairi Bongo Mrisho Mpoto, ameitaja sababu ya watu wengi kuachana na wapenzi wao ni pamoja na kuwaonesha kwenye mitandao ya kijamii.

Pichani ni Mrisho Mpoto

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Mrisho Mpoto amefunguka na kusema watu wanapenda kuwaonesha wapenzi wao mitandaoni, hali ya kuwa watu wao sio wamitandaoni na ikitokea mtu ana maneno matamu anaweza akamshawishi mpenzi wako kukusaliti.

"Unapokuwa na mahusiano au kwenye ndoa jua kabisa hayo ni maisha yenu sio instagram, kama mtu wako sio mtu wa mitandaoni usimuoneshe huko, kwa sababu watu hutumia maneno kutongoza na unapomshawishi mpenzi wako haimaanishi kama una maneno matamu kuliko wengine" amesema Mrisho Mpoto.

Mrisho Mpoto ameongeza kusema "Tumeona mahusiano yamepotelea instagram, facebook kwa sababu ya kutafuta wafuasi 'followers', kingine watu wanadhani wapenzi wao wanapenda kufanya mapenzi, utakuta wengine wanatumia hadi madawa ishu ni kuwa mtulivu kwenye mahusiano yako".

Pia amesema yeye yupo na mke wake kwa takribani miaka 18 sasa ila hata siku moja hajawahi kumuonesha mitandaoni kwa sababu anajua kuna mambo ya familia na kazi.