Saida Karoli awachana wenzake.

Tuesday , 12th Sep , 2017

Msanii wa muziki wa kike kutoka Tanzania Saida Karoli, ambaye sasa amerudi kwa kishindo baada ya kimya kirefu amewatolea uvivu wasanii wachanga wa kike wenye tabia za kujikweza na kujiona bora zaidi ya wenzao, na kusema tabia hiyo inakera kila mmoja.

Saida Karoli

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Saida Karori amesema tabia hiyo haifai kwani bado wana safari ndefu kwenye muziki, hivyo wasipokuwa makini watakosa hata watu wa kuwaokota pale ikitokea wakianguka.

"Kwa kweli hilo suala ni kero, na siyo tu kwangu, ni kero kwa ujumla, na siyo nzuri kwa sababu inasababisha mtu unashuka ghafla, mtu unapokuwa na upendo halafu hujisikii, wale uliokuwa ukiongea nao siku za nyuma ndiyo wanaku-suport kukubeba unapoanguka, hiyo ni tatizo kwao", amesema Saida Karoli.

Kwa muda mrefu Saida Karoli alikuwa nje ya 'game', lakini sasa amerudi huku akiwa ameachia kzi mpya mbili, na yuko mbioni kufanya collabo na msanii Eddy Kenzo wa Uganda.