Sheikh Yahaya amtabiria Dimpoz makubwa

Alhamisi , 21st Feb , 2019

Mtoto wa mtabiri maarufu Tanzania, Maalim Hassan Sheikh Yahaya Hussein, ametoa utabiri wake juu ya msanii Ommy Dimpoz, na kusema kwamba msanii huyo atainuka tena kwa spidi kubwa ziadi, na kazi zake zitafanya vizuri.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet  Bongo ya East Africa Radio, Maalim Yahaya amesema kwamba ingawa Ommy Dimpoz watu walishamkatia tamaa, lakini msanii huyo atawashangza wengi pale atakapoinuka, na wale wanaomsema vibaya hawataamini kitakachotokea.

“Ommy Dimpoz tena walikuwa wanamtabiria vibaya, ndio atakuja ataibuka vibaya sana, kwa sababu watu wanamuona anakwenda shimoni lakini atarudi vizuri, nyota yake ni mapacha, mapacha asili yake ni upepo na upepo uko flexible, huwezi kupumua bila hewa, namtabiria Ommy ataibuka sana, na wale waliokuwa wanamsemea vibaya watashangaa”, amesema Maalim yahaya.

Sambamba na utabiri huo, Maalim Yahaya amewatabiria wasanii wakubwa kufanya vizuri zaidi kwa mwaka huu, hata wale ambao wanachipukia watakuwa zaidi na kuwafunika wale wakubwa.

“Wasanii watapata tuzo hasa wale wakubwa, mfano Alikiba anaonekana atakwenda juu zaidi, Jaydee atakuwa very strong akitoka atatoka vizuri sana, na wasanii wengine”, amesema Maalim Husein.

Mtabiri huyo amesema kwamba mwaka huu licha ya mafanikio watakayoyapata wasanii, pia utakuwa mwaka wa maafa kwao kutokana na kuwa mwaka mgumu.