Shilole amtaka Nay wa Mitego kuacha tabia hii

Jumanne , 7th Jan , 2020

Msanii na mfanyabiashara Shilole, amefunguka na kusema Nay wa Mitego ana utamaduni wa kuwachana watu kwenye nyimbo zake, ila anatakiwa abadilishe aina ya muziki, aache kuchamba watu azungumzie nyimbo zinazohusu jamii.

Kwenye picha ni Shilole na Nay wa Mitego

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Shilole amesema, endapo Nay wa Mitego atam diss kwenye nyimbo zake atamwambia kuwa hataki mambo hayo kwa sababu yeye sio mtu wa HipHop.

"Nay wa Mitego ile ndiyo tamaduni yake tangu ameanza kuimba, huwa ana diss tu, kwahiyo ndivyo alivyo na huo ndio uhalisia wake, hatujawahi kumuona amebadilika na kuimba muziki mwingine anadhani huko ndipo pa kutokea, lakini anatakiwa abadilishe aina ya muziki aache kuchamba watu na aanze kuimba nyimbo ambazo zinazungumzia jamii" ameeleza Shilole.

Aidha Shilole ameongeza kuwa kama kuna msanii ambaye itamuuma endapo akizungumziwa na Nay wa Mitego kwenye nyimbo zake, basi amfuate amwambie, kama yeye alivyowaambia Rostam.