Jumatano , 9th Sep , 2020

Mfanyabiashara Uchebe amefunguka kinachondelea baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na aliyekuwa mkewe msaniii Shilole, ambapo amesema ametoa talaka za awamu hivyo anamtaka Shilole akae heda ili kupatiwa huduma na misingi mingine ya kuifuata.

Msanii wa Shilole na Uchebe

Akifunguka hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Uchebe amesema hawezi kusema kama ndoa ni mbaya kisa yake imeingia dosari kwa sababu ndoa ni jambo la kheri japo kama vijana wanakutana na mambo mengi.

"Matatizo yanaponikuta huwa namuomba sana Mungu nisifanye jambo la ajabu, maana wanawake wana vitu viwili kwanza anapomkosea mumewe hakubali anataka kushindana naye na kwenye ndoa ndiyo inawabeba sana" amesema Uchebe 

Aidha ameendelea kusema  "Mitahani ipo na inatokea ni moja ya hatua kwenye maisha, sasa hivi nimejipunguza kidogo sipo karibu na mwenzangu na nimetoa talaka ambazo zina awamu pia anatakiwa akae heda kupata huduma, ukitaka kuoa kuna misingi mingi unatakiwa kuifuata"