Jumapili , 17th Nov , 2019

Muigizaji wa Filamu Tanzania, Shamsa Ford amesema wanamuziki Ali Kiba n Ommy Dimpoz, hawana sifa za kuwa watuwanaopaswa kumuoa, kwa kile alichokidai hawanan sifa.

Muigizaji wa Filamu Tanzania, Shamsa Ford.

Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kwenye kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, ambapo amesema kwa sasa bado anatamani kuolewa hajakoma na akitokea mwanaume mwenye nia hiyo atakubali bila kusita.

"Ni kweli matamani kuolewa hata sijakoma na Mungu inshallah atanipa mume, ila kwa sasa sitaki kufanya makosa tena,nikiwa kama mtoto wakike nataka niwe mfano bora kwa wasichana wanaoniangalia, ikitokea kesho Mungu akinipa mume sahihi naiolewa sijakoma."

"Kati ya Ali Kiba, Marioo, na Ommy Dimpoz hakuna hata mmmoja mwenye sifa za kuwa mume wangu" ameongeza Shamsa Ford

Hivi karibuni Msanii huyo wa Maigizo alisema, kutokana na uzuri alionao, anaamini mwanaume anayetaka kumuoa kwa sasa anapaswa kutoa mahari ya shilingi Milioni 20.