
Msanii Killy
Harmonize ametangaza ujio wa mwimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa instagram, huku akisema Juni 2, 2021 ni #KillyDay, akiwa na maana ndio tarehe rasmi ya Killy kuachia kazi yake tangu ajiunge na familia ya Konde Gang.
Inahisiwa kuwa huenda Killy akaachia album yake kwani Mei 3 mwaka huu, Harmonize alitudokeza kuwa album ya Killy imekamilika na tayari ana video 6 mkononi kutoka kwenye album hiyo.